
KLABU ya Man United imemkaribisha aliyewahi kuwa nyota wao, Cristiano Ronaldo ambaye anatajwa kurejea tena kwa Mashetani Wekundu.
Manchester United imeripoti kuwa tayari Klabu ya Juventus wameipokea na kukubali ofa yao yenye thamani ya pound milioni 25 kwa ajili ya kumbeba Cristiano Ronaldo, taarifa hizi zimekuja muda mfupi tu baada ya Manchester City kutajwa kujiondoa kumuwania CR7.

