
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, limewasimamisha wabunge wawili, Jerry Silaa na Josephat Gwajima, kuhudhuria mikutano miwili ya bunge ambapo watarejea bungeni Januari, 2022.
Akisoma uamuzi huo, Spika Ndugai amesema kwa kipindi chote watakachokuwa wamesimamishwa, hawatatakiwa kufika katika eneo la bunge bila ridhaa ya Spika, na kwamba watakuwa wakipokea nusu ya mishahara na posho zao mpaka watakapomaliza kutumikia adhabu hizo.
Hatua hiyo ya Ndugai, imekuja baada ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kuwakuta na hatia wabunge hao katika tuhuma zilizokuwa zikiwakabili za kusema uongo na kushusha hadhi ya bunge na kutoa mapendekezo kwa spika kuwachukulia hatua za kinidhamu.