×

Simba Kuzindua Jezi Jumamosi Septemba 4 -Video

MKUU wa kitengo cha habari na mawasiliano Simba, Ezekiel Kamwaga leo Septemba 1, 2021 akiongea na wanahabari katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam amesema timu yake inakwenda kuzindua jezi za aina yake kupitia kwa muwekezaji wao Mkurugenzi wa kampuni ya Vunja Bei, Fred.

 

“Tuko hapa kuzungumza kuhusu jezi zetu mpya ambazo zitatolewa na mzabuni wetu mpya kampuni ya Vunja Bei.”-amesema Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano, Ezekiel Kamwaga

“Uzinduzi wa jezi za Simba tutafanya Jumamosi Septemba 4, 2021 saa 1:00 usiku kwenye hoteli ya Hyatt Regency. Litakuwa tukio ambalo litahusisha wadau mbalimbali, pia tutakuwa live kupitia Azam TV.”

 

“Jambo moja naweza kusema ni jezi nzuri sana. Tutakuwa na jezi za aina tofauti sana ukilinganisha na timu zingine za ndani. Baada ya uzinduzi jezi zitakuwepo kwenye maduka ya Vunja Bei na tutauza masaa 24.” amesema Mkurugenzi wa kampuni ya Vunja Bei, Fred

Leave a Comment