
Bi. Flora Andrea ambae ni mama mzazi wa aliyekuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Hayati Elias Kwandikwa amefariki wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Kahama, Mkoani Shinyanga.
Kifo cha Bi. Flora kimetokea ikiwa mwezi mmoja tu tangu kufariki kwa mtoto wake huyo ambae alikua Waziri wa Ulinzi.

Mwanafamilia ambae pia alikua Katibu wa Mhe. Kwandikwa, Julias Lugobi amethibitisha kwamba Bi. Flora alikuwa akisumbuliwa na tatizo la mapafu na alilazwa katika hospitali kwa muda wa wiki moja akipatiwa matibabu kabla umauti haujamkuta.
Mwenyezi Mungu ailaze mahala pema peponi roho ya Bi. Flora Andrea, AMEN!