×

Gazeti la Amani Lawapagawisha Watu Dar

Amani (1)     

Mohamed Mrisho mkazi wa Vikindu akisoma kwa makini gazeti la Amani.

Amani (2)
Omari mkazi wa Vikindu akifuatilia kilichoandikwa kwenye gazeti la Amani, kulia ni Afisa Usambazaji, Yohana Mkanda.

Amani (3)
Mama Nakombo mkazi wa Vikindu akiwa na Afisa Usambazaji, Jimmy Haroub akisoma Amani.

Amani (4)
Afisa Usambazaji, Jimmy Haroub (katikati) akiwa na masela Mohamed na Ali wakazi wa Vikindu wakisoma Amani.

Amani (5)
Wakazi wa Vikindu wakilishambulia gazeti la Amani kwa kulinunua na kuona kilichoandikwa.

Amani (6)
Mama Lishe wa Vikindu wakisoma Gazeti la Amani, katikati ni afisa usambazaji.

Wakazi wa maeneo  ya Vikindu mkoani Pwani leo wamejikuta wakipagawa vilivyo baada ya Gazeti la Amani kutua mtaano kwao hali iliyowasababisha kuzingira gari la matangazo kila mmoja akitaka kulisoma.

Afisa Usambazaji wa Global Publishers walifika eneo hilo la Vikindu na kuanza kuliuza gazeti hilo ambalo lina habari kubwa inayohusu waraka waliouacha magaidi kwenye nyumba iliyopo maeneo hayo ambapo kutokana na habari hiyo kuwavuta wengi walijikuta wakiacha kazi zao na kukimbilia kwenye gari kulinununua gazeti.

“Dah, hii habari inasisimua sana na imetokea hapahapa maeneo ya Vikindu ndiyo maana tumejikuta tukilikimbilia gazeti ili tuone kinachoendelea kwa kweli,” alisema Mohamed Mrisho mkazi wa Vikindu.

Stori/picha: Gladness Mallya/GPL

Leave a Comment