
MWANAFUNZI wa kidato cha tatu katika Shule ya Sekondari Kachwamba wilayani Chato, Keflin Charles (17) anatuhumiwa na Jeshi la Polisi kwa Kosa la kumtupa mtoto wake wa kiume aliyejifungua.
Imeelezwa kuwa, mwanafunzi huyo alimtupa mtoto wake huyo mchanga katika maeneo ya Shule Msingi Igalula, Kata ya Kasenga, baada ya kutelekezwa na mwanaume aliempa ujauzito huo.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita, ACP Henry Mwaibambe anasema baada ya jeshi hilo kufanya uchunguzi ndipo walibaini kuwa binti huyo ndiye aliefanya tukio hilo la kinyama.
Aidha, Kamanda Mwaibambe ametoa wito kwa wananchi kuacha vitendo vya ukatili badala yake watafute njia mbadala ili kupata suluhu ya changamoyo zinazowakabili.
View this post on Instagram