
KLABU ya Fountain Gate Princess imefanikiwa kutimiza lengo la kucheza mchezo wa kirafiki na Gairo Veterans, ikiwa ni katika jitihada za kuunga mkono juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan kuhamasisha watu kupata chanjo ya UVICO-19.
Fountain walishinda mabao 6-3 kwenye mchezo huo uliochezwa wikiendi iliyopita kwenye uwanja wa CCM Gairo.
Taasisi ya Fountain Gate Academy iliandaa tamasha maalum la kuhamisha watu kupata chanjo kwa hiari.
Mkurugenzi wa Fountain Gate Academy, Japhety Makau aliliambia Championi Jumatatu kuwa: “Tuliandaa tamasha hili lengo ikiwa ni kuhamasisha watu kuchanja kwa hiari na lengo letu ni kupata watu 1,000 waliochanjwa. Mechi hii ilikuwani sehemu ya hamasa.”
ISSA LIPONDA, Dar es Salaam