
YANGA ipo katika maandalizi ya mwisho ya mchezo wa hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Rivers United ya nchini Nigeria.
Mchezo huo unatarajiwa kupigwa Jumapili hii saa kumi na moja jioni kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam, huku Yanga wakipewa nafasi kubwa ya kushinda.
Yanga chini ya Kocha Mkuu raia wa Tunisia Nasreddeni Nabi tayari imefanya maandalizi ya kutosha katika kuelekea pambano hilo kwa kupata kikosi cha kwanza kitakachompa ushindi na kusonga mbele katika michuano hiyo mikubwa Afrika.
Nabi katika maandalizi yake ya mchezo huo dhidi ya River ameonekana akiwatumia na kuwapa maelekezo baadhi ya wachezaji wake waliokuwepo katika mipango yake.
Achana na katika mazoezi, pia kocha huyo ameonekana akiwatumia wachezaji wake hao kwenye michezo ya kirafiki miwili ya kirafiki waliyocheza dhidi ya Zanaco ya Zambia waliofungwa mabao 2-1 na ule wa Friends Rangers walioshinda 3-1, achana na ule wa jana dhidi ya Pan African.
Wapo baadhi ya wachezaji ambao hawakutumika katika michezo ya kirafiki kama vile Mganda, Khalid Aucho aliyekuwa katika majukumu ya timu ya taifa ambaye ana nafasi kubwa ya kui
Kikosi cha Yanga ambacho huenda Nabi atakitumia katika michuano hiyo ya kimataifa ambacho kinatarajiwa kuwepo na mabadiliko ya kumchezesha beki wa kushoto Kibwana Shiomari ambaye msimu uliopita alikuwa akimtumia beki wa kulia namba mbili.
Kikosi hicho cha kwanza cha Yanga kinatarajiwa kuwa hivi; kipa Djigui Diarra mabeki, Shaban Djuma, Shomari Kibwana, Yannick Bangala Litombo, Dickson Job.
Viungo, Khalid Aucho, Jesus Moloko, Mukoko Tonombe huku washambuliaji wakiwa Heritier Makambo, Feisal Salum ‘Fei Toto’ na Yacouba Songne.
Hicho ndiyo kikosi full ambacho kocha huyo atakitumia katika michuano hiyo ya kimataifa ambacho anaendelea nacho kukisuka kwa kuwapa mbinu mbalimbali katika mazoezi yake huko kambini Kijiji cha Avic Town, Kigamboni nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
Timu hiyo juzi ilituma orodha ya majina 28 ya wachezaji wao watakaowatumia katika michuano hiyo ambao ni, Erick Johora, Ramadhani Kabwili. Mabeki wa pembeni ni Djuma, Kibwana, Paul Godfrey, Yassin Mustapha, Adeyum Saleh na David Bryson.
Wengine ni Litombo, Job, Bakari Mwamnyeto na Abdallah Shaibu ‘Ninja’. Viungo ni Aucho, Tonombe, Feisal Salum na Zawadi Mauya, Fei Toto.
Moloko, Fei Toto, Farid Mussa, Deus Kaseke, Mapinduzi Balama na Dickson Ambundo. Washambuliaji ni Makambo, Diston Mayele, Ditram Nchimbi na Yusuph Athumani.
WILBERT MOLANDI, Dar es Salaam