×

Ambundo Ajipa Kazi Ngumu Yanga SC

WINGA wa Yanga, Dickson Ambundo, amejipa kazi ngumu ndani ya kikosi hicho ikiwa ni pamoja na ile ya kuona timu hiyo inatwaa mataji na kufanya vizuri katika Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu.

 

Ambundo ni nyota mpya ndani ya kikosi hicho ambapo aliibuka huko akitokea Dodoma Jiji inayonolewa na Kocha Mkuu, Mbwana Makata.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Ambundo alisema kuwa kazi yake kubwa ni kuona anashirikiana
na wachezaji wengine ili kufikia
malengo ambayo wameweka.

 

“Tuna kazi kubwa ya kufanya hiyo ni lazima iweze kukamilika, kwenye ligi tuna malengo ya kufanya vizuri kwa kupata matokeo chanya na hata kwenye mashindano ya kimataifa ni muhimu kufanya vizuri.

 

“Ushindani utakuwa mkubwa hilo lipo wazi lakini nasi lazima tutapambana kupata matokeo kwenye mechi zetu ambazo tutacheza, mashabiki wawe bega kwa bega nasi,” alisema Ambundo.

LUNYAMADZO MLYUKA

Leave a Comment