×

Gomes Ampa Sakho DK 270 tu Simba SC

KOCHA Mkuu wa Simba, Mfaransa, Didier Gomes, ameomba mastaa wake awapime kwa kucheza mechi tatu za kirafiki ambazo ni sawa na dakika 270 kabla ya kukutana na TP Mazembe ya DR Congo.


Simba kwa sasa ipo
Arusha katika kambi ya kujiandaa na msimu wa 2021/22 ambapo ikiwa huko imepanga kuchezea michezo hiyo kabla ya kurudi Dar kukabiliana na TP Mazembe, kwenye Tamasha la Simba Day, Septemba 19, mwaka huu.

 

Mastaa ambao tangu Jumatatu ya wiki hii wapo kambini Arusha ni pamoja na Papa Ousmanne Sakho ambaye ni ingizo jipya kikosini hapo, huku akianza kwa moto.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Mratibu wa Simba, Abbas Ally, alisema kocha huyo amepanga kucheza michezo hiyo mitatu ya kirafiki maalum kwa ajili ya kutengeneza muunganiko wa timu ambayo itakuwa na uwezo wa kucheza vizuri na kuelewana.

Ally alisema kuwa mchezo wao wa kwanza walitarajiwa kucheza jana Jumatano jioni dhidi ya Coastal Union ya Tanga.

 

“Awali tulipanga kucheza michezo mitano ya kirafiki kabla ya kurejea Dar kucheza dhidi ya Mapembe katika Tamasha la Simba Day.“Lakini kutokana na ratiba kutubana, tutacheza michezo mitatu pekee ya kirafiki na mmoja tutacheza leo (jana) jioni dhidi ya Coastal Union ya Tanga.

 

Baada ya mchezo huo, itajulikana timu nyingine tutakayocheza nayo hapo baadaye, mazungumzo yanakwenda vizuri na baadhi ya timu zilizoonesha nia ya kucheza dhidi ya Simba,” alisema Ally.

STORI NA WILBERT MOLANDI, Dar es Salaam

Leave a Comment