
Cristiano Ronaldo amerejea Manchester United. Akiwa na kapu la mabao na kukusanya makombe lukuki tangu aondoke Old Trafford, mshambuliaji wa Ureno amerejea tena kwa mashetani wekundu.
Kushinda taji la kwanza la Ligi kuu (2007)
“Mwanzoni, hakuna aliyekuwa amewahi kumsikia Ronaldo, lakini mwishowe, kila mtu alikuwa anamjua.”
Hayo yalikuwa maoni ya mlinzi wa zamani wa Manchester Mikael Silvestre, aliyecheza mchezo dhidi ya Sporting Lisbon katika mechi za kujiandaa na msimu wa 2003-04.
Ronaldo alishawishiwa kujiunga na klabu ya Manchester na Sir Alex Ferguson baada ya kuonyesha kiwango cha hali ya juu katika mchezo huo wa kirafiki – na kwenda kuichezea United michezo 292, akishinda taji la kwanza kati ya matatu ya ligi kuu England mwaka 2007, pamoja na ligi ya mabingwa, Kombe la FA na makombe mawili ya kombe la ligi.
Tuzo ya Puskas ya goli bora (2009)
Ronaldo ameifungia Manchester United mabao 118, likiwemo goli zuri dhidi ya Porto katika ligi ya mabingwa Ulaya, akifunga goli hilo kwa shuti gali lililojaa kwenye pembe ya goli kutoka umbali wa yadi 40. Goli hilo likashinda tuzo ya FIFA ya Puskas ya goli bora la mwaka duniani.
United ikafika fainali yake ya pili mfululizo lakini ikafungwa na Barcelona katika mechi ya mwisho ya Ronaldo kabla ya kukamilisha uhamisho wake wa thamani ya £80m na kutua Real Madrid msimu huo.
Goli la ushindi kwenye fainali ya kombe la Copa del Rey (2011)
Ronaldo akiruka kichwa kuifungia Real Madrid bao la ushindi katika dakika za nyongeza dhidi ya Barcelona. Dau la uhamisho lililowekwa rekodi ya dunia la Ronaldo lilianza kulipa pale alipoifungia goli la ushindi Real Madrid katika mchezo wa fainali ya Copa del Rey dhidi ya mahasimu wao wakubwa.
Ronaldo aliruka juu na kufunga goli hilo la kipekee akiunganisha krosi ya Angel di Maria na kutwa akombe lake la kwanza akiwa ana klabu hiyo
Kuwa mfungaji bora wa muda wote wa Real Madrid (2015)
Rekodi ya upachikaji wa mabao wa Ronaldo katika misimu tisa akiwa Real Madrid ilikuwa ya kushangaza, akifunga mabao 450 katika michezo 438.
Goli lake dhidi ya Levante kwenye mchezo uliochezwa oktoba 2015, ulimfanya Ronaldo kuwa mfungaji bora wa muda mote wa Real Madrid, akimpiku Raul mwenye mabao 323.
Msimu wa nyuma yake wa 2014-15 ulikuwa msimu mzuri zaidi katika maisha yake kwenye klabu hiyo, akifunga mabao 61 katika michezo 54, kwa wastani wa bao moja katika kila dakika 76.
Kutwaa taji la Euro akiwa na Ureno (2016)
Ronaldo finally tasted success on the international stage with Portugal, winning the 2016 European Championship with victory over France in the final in Paris.
Tuzo ya Ballon d’Or imetolewa mara 62, – Cristiano Ronaldo akishinda mwaka 2008, 2013, 2014, 2016 na 2017. Mwaka 2008, 2013, 2014, 2016 na 2017, Ronaldo alitwaa tuzo ya Ballon d’Or ya mchezaji bora wa dunia.
Tuzo ya mwaka 2017 ilikuja kufuatia msimu mzuri aliokuwa nao wa 2016-17 ambao alifanikiwa kutwaa taji la ligi kuu ya Hispania, La liga na ushindi katika fainali ya ligi ya mabingwa ulaya, ambapo Ronaldo alifuunga mabao mawili katika ushindi wa 4-1 dhidi ya Juventus.
Kufikisha karne ya mabao ya ligi ya mabingwa Ulaya (2018)
Ronaldo alikuwa mchezaji wa kwanza kufikisha mabao 100 ya ligi ya mabingwa Ulaya, kabla ya hasimu wake mkubwa Lionel Messi kuungana nae.
Mabao yake mawili dhidi ya Paris St-Germain katika hatua ya 16 bora ya michuano hiyo yalimfanya kuvuka mstari wa karne ya mabao (kwa maana ya mabao 100) na kusalia kuwa mfungaji bora wa muda wote wa michuano hiyo akiwa na mabao 134 katika michezo 176.
Goli la ‘Bicycle kick’ dhidi ya Juventus (2018)
Lilikuwa goli tamu na la kipekee na namna meneja wa Real Madrid Zinedine Zidane’s alivyolipokea ni ishara tosha. Zidane aliweka mikono yake kichwani, haamini anachokiona. Ronaldo aliluka hewani kabla ya kutandikwa mkwaju huo na kujaa nyavuni kwenye kona kwa kutumia ‘bicycle kick’.
Goli hilo kwenye robo fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya lilikuwa zuri kiasi cha hata mashabiki wa Juventus walisimama na kumpigia makofi mchezaji huyo, ambaye baada alijiunga na klabu yao (Juve).
Mchezaji wa kwanza kutwaa mataji matano ya ligi ya mabingwa Ulaya (2018)
Ronaldo alishinda mataji mawili ya La Liga na mawili ya Copa del Rey akiwa na Real Madrid, lakini kushinda mataji ya Ulaya kukamfanya kuwa gwiji wa kweli wa soka.
Alikuwa ameshashinda taji la mabingwa Ulaya akiwa na United mwaka 2008, lakini akaenda kushinda manne mengine akiwa na Real Madrid.
La kwanza lilikuwa mwaka 2014 kabla ya kushinda matatu mfululizo mwaka 2016, 2017 na 2018 na kuwa mchezaji wa kwanza kushinda mataji matano ya ligi ya mwabingwa Ulaya.
Rekodi ya mfungaji bora wa muda wote wa mabao timu za taifa (2021)
Mapema mwaka huu Ronaldo aliifikia rekodi ya kufunga mabao mengi kwenye timu ya taifa, akifikisha jumla ya mabao 109 alipoifungia Ureno mabao mawili ya penati katika mchezo wa sare ya 2-2 dhidi ya Ufaransa.
Mabao hayo yalifanya aifikie rekodi iliyowekwa na Ali Daei wa Iran ya mwanasoka wa kiume aliyefunga mabao mengi akiwa na timu ya taifa. Daei ana mabao 109 aliyoyafunga kati ya mwaka 1993 na 2006.
Lakini mabao yake mawili (bao la 110 na 111) aliyoyafunga wiki hii dhidi ya Jamhuri ya Ireland yamemfanya kufikisha mabao 111 na kumfanya nyota huyo mwenye umri wa miaka 36 kuwa mfungaji bora wa muda wote wa mabao kwa timu za taifa.