×

Mashabiki Wamiminika Kuwapokea Mabingwa wa Kombe la Shirikisho Dar – (Picha +Video)


Ni mwendo wa shangwe na furaha katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, ambapo mashabiki na viongozi mbalimbali wa Simba leo Julai 5, 2026 wamejitokeza kwa wingi kuipokea timu yao iliyowasili kutoka Pemba, baada ya kutwaa Kombe la Shirikisho.

Timu hiyo iliwasili jijini Dar es Salaam ikitokea visiwani Zanzibar, ambapo ilifanikisha ushindi wa kihistoria na kuibuka mabingwa wa michuano hiyo. Mara baada ya kutua, wachezaji walipokelewa kwa nderemo, vigelegele na shamrashamra kutoka kwa mashabiki waliokuwa wamejazana uwanjani hapo.

Baada ya mapokezi hayo, msafara wa timu ulianza rasmi parade maalum kupitia mitaa mbalimbali ya jiji, ukiwa ni sehemu ya kusherehekea ushindi huo mkubwa uliowapa heshima mpya katika soka la nchini.

Shughuli hiyo imeelezwa kuwa ni moja ya mapokezi makubwa ya michezo kushuhudiwa hivi karibuni, ikionyesha namna mashabiki walivyoguswa na mafanikio ya timu yao.

Leave a Comment