×

Mbunge Aliyeteuliwa na Rais Samia Aapishwa

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai leo Septemba 10, 2021 amemuapisha Dkt. Stergomena Tax kuwa mbunge baada ya kuteuliwa na rais mapema hii leo.

Dk. Tax ameteuliwa leo na Rais Samia Suluhu Hassan kutoka katika nafasi kumi za wabunge wa kuteuliwa na rais ambapo kabla ya uteuzi huo, alikuwa Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) ambapo amemaliza muda wake Agosti, mwaka huu.

Leave a Comment