×

Waziri Kigahe Azindua TATA Intra V20 Suluhisho la Uchukuzi

Naibu Waziri, Exaud Kigahe akiikagua gari hiyo.

 

 

 

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe amezindua gari ndogo ya mizigo aina ya Tata Intra V20 inayotengenezwa na Kampuni ya Tata Motors ambayo imetajwa kuwa suluhisho la shughuli ndogondogo za uchukuzi mizigo na shughuli zingine za usafirishaji.

Naibu Waziri Kigahe (katikati) na wadau baada ya uzinduzi.

 

 

Uzinduzi huo umefanyika Hoteli ya Hyatt Regecy, The Kilimanjaro Hotel, Jijini Dar na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali.

Sehemu ya wageni waalikwa wakishuhudia uzinduzi huo.

 

 

Akizungumzia ubora wa gari hiyo wakati wa uzinduzi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Tata Africa Holdings Ltd, Mr. Niraj Srivastava, amesema pamoja na uimara wake ina injini yenye nguvu na inaimiri mazingira ya kitanzania ikiwemo sehemu zenye barabara za viwango tofauti.

Mkurugenzi Mtendaji wa Tata Africa Holdings Ltd, Mr. Niraj Srivastava.

 

 

Mr. Niraj amesema uwezo wake ni kubeba tani 1,100 sawa na tani moja na kilo 100 huku matumizi yake ya mafuta ikiwa ni kidogo sana ukilinganisha na magari mengine jambo linaloweza kuwaongezea kipato wamiliki wa gari hiyo.

 

 

“Toleo hili ya Tata Intra V20 litakuwa suluhisho la shughuli ndogondogo za uchukuzi hapa nchini ikiwemo ubebaji wa mizigo na matumizi mengine ya usafirishaji.

 

 

Sifa nyingine ya gari hii ni imara na inatumia mafuta kidogo kwa umbali mrefu jambo litakalookoa kipato cha mtumiaji na kumfanikisha katika mapambano ya kimaendeleo” alisema Mr. Niraj.

 

 

Waziri Kigahe akizungumza baada ya uzinduzi huo aliishukuru kampuni hiyo kwa uwekezaji wake huo hapa nchini na kusema ujio wa gari hizo anaamini utaongeza fursa za ajira na ongezeko la kodi katika shughuli mbalimbali zitakazokuwa zikifanywa na magari hayo.

 

 

Niwapongeze Kampuni ya Tata Motors kwa uwekezaji wenu huu na magari haya ambayo naamini yatakwenda kutatua changamoto mbalimbali za usafishaji na kama mlivyojielezea kuwa hata umiliki wake ni rahisi.

 

 

“Nawaunga mkono kwa kutuletea magari haya ambayo naamini yataongeza hata fursa za ajira hapa nchini,” alimaliza kusema Waziri Kigahe.

 

 

Uzinduzi huo ulihudhuriwa na wadau wengine mbalimbali akiwemo Mkurugenzi Mtendaji wa Tata Africa Holdings Ltd Mr. Niraj Srivastava, Meneja Mwandamizi Kitengo cha Biashara Tata Motors Ltd, Mr. Asif Shamim na wengineo.

Leave a Comment