×

Ligi ya Mabingwa Imemshinda Solskjaer

KIPIGO kisichotarajiwa cha mabao 2-1 dhidi ya Young Boys, kimemfanya kocha wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer kuwa mdebwedo kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Takwimu za Opta, zinaonyesha kuwa, kocha huyo sasa amepoteza mechi saba kati ya mechi 11 alizoiongoza United kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Alifungwa na PSG, akafungwa na Barcelona mara mbili msimu wa 2018-19 na kupoteza mechi tatu kati ya sita za hatua ya makundi msimu uliopita, kabla ya kupoteza dhidi ya Young Boys ya Uswisi juzi.

United wana asilimia 13 ya vipigo katika historia ya michuano hiyo, na asilimia kubwa kati ya hizo, timu hiyo ilikuwa chini ya Solskjaer, licha ya kuongoza kwa asilimia tano tu ya mechi hizo.

Solskjaer alianza kuinoa United Desemba 2018 kufuatia kutimuliwa kwa Jose Mourinho. Presha imeanza kuwa kubwa kwa Solskjaer hasa baada ya kuwasajili wakali Jadon Sancho, Raphael Varane na Cristiano Ronaldo.

Leave a Comment