×

Owen: PSG ya Messi ni Dhaifu

MICHAEL Owen anadai kikosi cha Paris Saint-Germain ni dhaifu sasa baada ya Lionel Messi kujiunga na klabu hiyo kufuatia Muargentina huyo kushindwa kufunga bao kwenye mechi yake ya kwanza akianza katika timu hiyo.

 

Messi alianza mechi hiyo ya kwanza ya PSG kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu dhidi ya Club Bruges juzi Jumatano, sambamba na Kylian Mbappe na Neymar, lakini hakuna hata mmoja kati ya masupastaa hao aliyefunga kwenye sare hiyo ya bao 1-1 ugenini.

 

Utatu huo mtakatifu ambao media za Ufaransa zinauita ‘MNM’, ndio utatu unaovutia zaidi katika ulimwengu wa soka, lakini mchambuzi Owen amesema haitoshi kuifanya PSG ipewe nafasi ya kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya.

 

“Hii timu ya PSG, na mafowadi hao, ni bora sana kwa sasa. Lakini watatu hawa pamoja wanaifanya iwe dhaifu kwangu mimi na sijui kwa nini ni moja ya timu zinazopewa nafasi (kutwaa taji la Ulaya). Nadhani timu za England (Chelsea, Liverpool, Manchester City na Man United) ni bora zaidi yao, kwa mbali sana.”

 

PSG pia wana Manchester City na RB Leipzig katika kundi lao, huku wakitarajiwa kukabiliana na vijana wa Pep Guardiola katika mchezo wao unaofuata Uefa.

LONDON, England

Leave a Comment