
WAWAKILISHI wa Tanzania kwenye ligi ya mabingwa Afrika, Yanga leo Septemba 19, imetupwa nje ya michuano hiyo baada ya kupoteza mchezo wa ugenini dhidi ya Rivers United ya Nigeria.
Yanga imepoteza kwa jumla ya Magoli 2-0 baada ya kupoteza mchezo wa kwanza kwa bao 1-0 uliochezwa uwanja wa Benjamin Mkapa Dar.