
MTU mmoja anayefahamika kwa jina la Miringa James amejikuta mikononi mwa vyombo vya ulizni na usalama nchini baada ya kutaka kutapeli akijifanya kuwa yeye ni afisa wa kukusanya Mapato kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Tukio hili limetokea jana Jumanne, Septemba 21, 2021 maeneo Bunju mkoani Dar es Salam ambapo baada ya kunaswa alikiri kwa kinywa chake kutenda kosa hilo huku akiomba msamaha na kusema hatarudia tena. Hata hivyo, Jeshi la Polisi linamshikilia kwa mahojiano zaidi na hatua zaidi za kisheria.
TAZAMA VIDEO ALIVYONASWA