×

Benki ya Dunia Kushirikiana na Tanzania Kukuza Uchumi

RAIS wa Benki ya Dunia (World Bank) David Malpass amesema Benki hiyo itaendelea kushirikiana na serikali kukuza uchumi kupitia mabadiliko ya kidigitali kwa kushirikiana na Sekta binafsi.

 

Ameeleza hayo alipokutana na kufanya mazungumzo na Rais Samia Suluhu Hassan ambaye ameishukuru (WB) kwa mchango wake kwa Tanzania kwenye huduma za Jamii na mapambano dhidi ya Covid- 19.

 

Pia, Rais amefanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Biashara Duniani (WTO), Ngozi Okonjo-Iweala kuhusu kuwezesha Biashara kwa kuimarisha upatikanaji wa Chanjo, usimamizi wa Uvuvi na Kilimo.

 

Rais Samia yupo New York,  Marekani akihudhuria mkutano wa 76 wa Umoja wa Mataifa.

Leave a Comment