Spika wa Bunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai, ametoa pole kwa familia, wabunge, ndugu, jamaa na marafiki kufuatia kifo cha mbunge wa Ngorongoro na Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji William Tate Ole Nasha, aliyefariki dunia jijini Dodoma.
Taarifa ya Spika Ndugai imetolewa leo Septemba 28, 2021, na Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Kimataifa, Ofisi ya Bunge, na kusema ofisi hiyo inafanya mawasiliano na serikali kuhusu ratiba za mazishi.
“Natoa pole kwa familia ya marehemu, serikali, wananchi wa jimbo la Ngorongoro, wabunge wote, ndugu na jamaa wa marehemu kwa msiba huu mkubwa,” imeeleza taarifa ya Spika Ndugai
