
WAZIRI Mkuu Kasimu Majariwa amechangia bati 200 mifuko ya simenti 150 na fedha tasilimu shilingi milioni 1 kwa wananchi wa jimbo la Kibiti Mkoani Pwani ikiwa ni mchango wake katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa wananchi. Akitoa taarifa kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa Wananchi wa jimbo la Kibiti katika mkutano wa kushukuru kwa ajili ya uchaguzi mkuu uliopita.
Mwakirishi huyo wa Mheshimiwa Waziri Mkuu ambaye ni Msaidizi wake jimboni alisema michango hiyo aliyoleta ni kutokana na mahusiano aliyofanya Mbunge wa jimbo la Kibiti Mheshimiwa Twaha Mpembenue ambaye alikuwa Das Wilaya ya Ruangwa hapo kabla ya kuwa Mbunge.
Mbunge wa jimbo la Kibiti Mheshimiwa Twaha Mpembenue amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutekeleza utekelezaji wa ilani ya miradi mikubwa kimkakati ya kitaifa na na ndani ya jimbo hilo.
Nae Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Pwani Mheshimiwa Subira Mgalu amewataka wananchi wa mkoa wa Pwani kuendelea kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan katika uzoefu wake wa uongozi unaendelea kunaonekana.