×

Anayedai Kuwa Mtoto Wa Mzee Yusuf Afiwa Na Meneja Wake-Video

Siku chache baada ya kijana mdogo, Hamad Hassan Mashauri mkazi wa Charambe Magengeni jijini Dar es Salaam kuibuka na kudai kwamba yeye ni mtoto wa mkongwe wa muziki wa Taarab nchini, Mzee Yussuf almaarufu Mfalme kisha msanii huyo kumkana, kijana huyo amepata pigo lingine.

 

Hamad ambaye pia ni msanii wa muziki wa singeli anayechipukia, amepata pigo hilo baada ya mtu aliyekuwa akimsimamia katika shughuli zake za muziki, Ramadhan Omary Chikawe, kufariki dunia kwa kugongwa na lori akiwa anaendesha pikipiki, tukio lililotokea Mkuranga mkoani Pwani.

 

Leave a Comment