
Kampumi za bima nchini zimetakiwa kuongeza Kasi ya utoaji wa elimu ya masuala ya bima kwa wananchi kabla ya kuwauzia bima hizo ili kuondokana na malalamiko yanayosabishwa na uelewa mdogo wa wanachama wao juu ya huduma na malipo yanayotakiwa kugharamia huduma husika.

Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Masoko, Mipango na Utafiti kutoka TIRA, Zacharia Muyengi wakati akizindua huduma mpya ya bima inayohusika na majanga ya udukuzi iliyoanzishwa na Kampumi ya Jubilee Insuraynce kukabiliana na wizi na uhalifu wa mitandao unaoendelea kushika Kasi katika maneo mbalimbali nchini na duniani kote.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa program za bima wa Kampumi hiyo amesema bima hiyo Ni bidhaa mpya anayolenga kulinda nyaraka na taarifa za makampuni zinazohifadhiwa kupitia mfumo wa mitandao mbalimbali Kama Google, Yahoo Gmail na mengineo