
MLINZI wa Kulia wa Simba Shomari Kapombe, ataukosa mchezo wa kesho wa ligi kuu Tanzania Bara dhidi ya Dodoma Jiji, mchezo utakaochezwa kwenye dimba la Jamhuri jijini Dodoma mishale ya saa 10:00 jioni.
Kocha msaidizi wa Simba amesema ukimuacha Kapombe wachezaji wengine wote wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa kesho ambao wanaamini utakuwa mgumu.
“Tunahitaji alama tatu kwenye mchecho wa kesho kutokana na matokeo ya mechi zetu tatu zilizopita ili kurudisiha ari kikosini pamoja na hamasa kwa mashabiki”
Beki huyo mwenye uwezo mkubwa wa kupanda na kushuka ataukosa mchezo huo kwa sababu ya majeruhi, mechi ya kwanza ya ligi ilibanwa mbavu na Biashara United