
SHOSHOLITI matata Bongo ambaye pia ni msanii wa Bongo Fleva, Irene Louis ‘Lyyn’ anasema kuwa, kwenye maisha yake hapendi mwanaume ambaye hana pesa hivyo kama mwanaume anajua hana pesa basi akae mbali naye.
Katika mahoiano maalum na Gazeti la IJUMAA, Lyyn ambaye ni zilipendwa wa Diamond Platnumz na Tommy Flavour anasema kuwa, yeye ni mwanamke anayependa vitu vizuri hivyo lazima awe na mwanaume mwenye kipato cha juu.
“Kwenye maisha yangu sipendi mwanaumwe asiyekuwa na pesa maana mimi napenda sana kuwa na vitu vizuri. Nataka mwanaume hata nikiumuomba milioni 10 anipe hapohapo siyo kuzungushana hivyo kama mwanaume hana pesa, basi akae umabli wa mita mia moja kutoka nilipo,” anasema Lyyn ambaye bado anakiwasha na ngoma yake ya Maneno.
STORI: KHADIJA BAKARI