
KUNA stori imevuja kwamba, Diamond Platnumz alipanga kumtumia mmoja wa ma-baby mama wake, Tanasha Donna kama video vixen (muuza sura) kwenye video yake mpya ya Naanzaje, lakini habari za ndani zinadai kuwa, mwanamama huyo alimtolea nje.
Dairekta wa video hiyo, Hanscana amethibitisha Tanasha kukataa dili hilo.
“Ni kweli mtu wa mwanzo kabisa ambaye alipaswa kuwepo kwenye shooting ya video ni Tanasha Donna. Diamond alimpigia simu, lakini siku iliyofuata alibadilisha mawazo na aliniambia tunapaswa kushuti na msichana kutoka Dubai,” anasema.
Diamond and Tanasha wamejaaliwa mtoto mmoja wa kiume, Naseeb Junior. Wakati wawili hao wakitoka kimapenzi walifanya wimbo wa pamoja uitwao Gere kabla ya mambo kwenda mrama na kila mmoja kuchukua hamsini zake.