
DAR ES SALAAM. Vodacom Tanzania Plc, inaendelea kusaidia mpango wa kuwezesha mapilo ya kidijitali nchini. Leo hii, kampuni unayoongoza ya teknolojia na mawasiliano imekabidhi reflekta zaidi ya 2,000 kwa Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) zitakazotumika na wakusanya malipo ya maegesho ya magari nchi nzima.

Hivi karibuni, TARURA ilizindua mfumo wa kidijitali wa malipo ya maegesho ya magari ili kuondoa ahda ya matapeli kuwabugudhi madereva, jambo ambalo limekuja kuwa kero katik miji mikubwa. Mfumo mpya unategemewa kuleta manufaa mengi kwa watumiaji wa barabara nchini.
Akizungumza wakati wa makabidhiano yaliyofanyika katika ofisi za TARURA Ilala, Dar es Salaam, Mkurugenzi wa M-Pesa wa Vodacom, Bw. Epimack Mbeteni alipongeza uamuzi wa TARURA kuondokana na malipo ya pesa taslimu, jambo ambalo siyo tu litaweka makusanyo yote mahali pamoja ila pia kuwapa watumiaji unafuu unaotokana na malipo ya kidijitali.
“Kama kampuni, malipo ya kidijtali imekuwa jambo tunalotangaza kila siku tangu tuanzishe mfumo wa LIPA kwa M-Pesa mwaka 2009 kuwezesha makusanyo na malipo ya makampuni ya biashara na serikali. Tunafurahi kuona taasisi nyingi Zaidi za serikali zikiingia mfumo wa kidijitali na hivyo kuteleta hatua moja karibu Zaidi kufikia jamii iliyondokana na matumizi ya pesa taslimu” alisema.
Vodacom tanznia imekuwa ikiisaidia serikali katika jitihada zake za kupunguza matumizi ya pesa taslimu nchini kwa kushirikiana na taasisi za serikali kuweza kutumia mifumo ya malipo kidijitali pamoja na kuelimisha watumiaji kuingia kwenye mfumo mpya unaotumia LIPA kwa M-Pesa.
“Malipo kwa TARURA yanaweza kutimizwa haraka kupitia M-Pesa ya Vodacom kwa kupiga namba *150*00# kuingia kwenye menu ya M-Pesa kisha kuchagua huduma husika, Napenda kuwahiimiza wateja wetu kuendelea kutumia huduma zetu za LIPA kwa malipo kwa taasisi za srikali, kwa wafanyabiashara na malipo mengine kwani malipo haya hayana tozo za serikali.”
Akipokea reflekta zilizotolewa na vodacom Tanzania, Mhasibu Mkuu wa TARURA Jacob Nyaulingo alitoa shukurani kwa msaada wa Vodacom katika mchakato mzima na alihimiza watu kutumia mfumo wa malipo kidijitali kwa tija na wepesi wake.
“Wahudumu wetu nchini watavaa reflekta hizi zinazoonekana kirahisi ili kutambulika haraka na kuweza kutoa msaada popote utakapohitajika kwani mfumo bado ni mgeni kwa wengi. Tunashukuru kwa msaada wa Vodacom katika jambo hili na tunategemea kushirikiana katika utekelezaji” alisema.