×

Bibi Mlemavu Alia Kuporwa Ardhi-Video

Bi Venansia Kasoli ni bibi ambaye licha ya ulemavu wake lakini bado anapambana vyema katika utafutaji wa mkate wa kila siku.

 

Makazi ya bibi huyu ni duni kutokana na nyumba yake kuanguka msimu uliopita wa mvua za mwaka jana huku akilazimika kuishi katika pagare hili japo kuwa ni hatari zaidi kwake.

 

Bibi venansia Kasoli anasema ulemavu wa miguu alionao kuna wakati unampa changamoto kuzifanya shughuli zake na kutofikia malengo aliyojiwekea katika utafutaji wa mkate wa kila siku.

 

Katarina Kibamba ni rafiki wa Bi Venansia Kasoli amemtembelea rafiki yake ili kumjuluia hali naye anakiri kuwa rafiki yake anakabiliwa na changamoto kubwa sana.

 

Hata hivyo uongozi wa mtaa huu wa mawelewele unakiri kuzitambua changamoto za bibi venansia ikiwemo changamoto ya kunyang’anywa eneo la mlemavu huyo.

Leave a Comment