×

Watanzania Zaidi ya 940,000 Wamechanjwa

MSEMAJI wa Serikali Gerson Msigwa amesema utoaji wa chanjo aina ya Johnson & Johnson umekamilika na kwa takwimu za hadi Ijumaa Oktoba 15, Watanzania zaidi ya 940,000 walikuwa wameshapata chanjo hiyo, kwa mujibu wa taarifa ya Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa, aliyoitoa leo  Oktoba 17, akiwa jijini Mwanza. Tanzania ilipokea dozi 1,058,400 za chanjo aina ya J&J kupitia mpango wa COVAX facility.

 

Msigwa amesema zoezi la utoaji chanjo linakwenda vizuri na tayari serikali imeshaongeza chanjo aina ya Sinopharm chini ya Mpango wa Shirika la Afya Duniani wa COVAX facility ambapo Tanzania imepata dozi 1,065,000. Tayari chanjo hizo zimeanza kupelekwa katika ngazi ya halmashauri ili zitolewe kwa wananchi.

 

amesema serikali itapokea dozi nyingine 500,000 ya chanjo aina ya Pfizer mwisho wa mwezi Oktoba, chanjo hizo ni sehemu ya dozi 3,700,000 ambazo Tanzania itapokea kupita mpango wa COVAX facility.

 

“Wale ambao wako tayari watapata chanjo. Chanjo hizi ni hiari na zitaendelea kuja awamu kwa awamu,” amesema na kusisitiza serikali imeweka majokofu 14 mkoani Dar es Salaam yenye uwezo wa kuhifadhi chanjo kwa nyuzi joto hasi 60 hadi 80. Majokofu hayo yanauwezo wa kuhifadhi chanjo zote dozi 3,700,000.

Leave a Comment