
WAKATI wewe ukipewa zawadi ya keki na maua katika mfanano wa siku yako ya kuzaliwa (Birthday), mwenzako Cardi B amezawadiwa jumba la kifahari katika siku yake ya kuzaliwa.
Mume wa Card B, Offset alitoa zawadi hiyo ya jumba la kifahari kwa baby mama wake huyo ambaye amemzalia watoto wawili, mapema Oktoba mwaka 2021.
Kwa Offset siyo jambo geni kumzawadia mke wake zawadi za kifahari kama hizo ila zawadi hii ni tofauti na zile alizowahi kumzawadia baby mama huyo.
Offset alimshangaza mke wake kwa zawadi hiyo huku akisikika akizungumza maneno machache kabla ya kumuonesha baby mama wake video fupi ya jumba hilo la kifahari, katika kipande cha video kinachosambaa mitandaoni Offset alisikika akisema:
“I done bought you the biggest diamonds you could get, I done bought you everything, so this year I wanted to buy something that means something. You gave me my beautiful son, I bought you a house in DR.” (Nimekununulia almasi za thamani kubwa, nimekununulia kila kitu, lakini mwaka huu nilihitaji nikununulie kitu ambacho kitaacha alama. Umenizalia mtoto mzuri wa kiume, na mimi nimekununulia nyumba huko DR)
Na Bakari Mahundu, Dar