
Polisi nchini Ghana wanafanya uchunguzi juu ya taarifa zinazosambaa mitandaoni, zikimuhusisha Staa wa Muziki nchini humo, Shatta Wale kupigwa risasi na kupelekea kifo chake Oktoba 18.
Taarifa za kupigwa risasi zilianza kusambaa kama njugu Jumatatu, kufuatia msaidizi wa karibu wa Shatta Wale, Nana Dope kutoa taarifa zinazohusiha mapigano ya risasi yaliyopelekea kujeruhiwa kwa boss wake (Shatta Wale) na kukimbizwa hospitalini akiwa na hali mbaya.
Ikumbukwe; Jumanne, Septemba 28 mwaka 2021 Mtumishi wa Mungu, Askofu Stephen Akwasi maarufu zaidi kama Jesus Ahoufe, aliwahi kutoa unabii juu ya kifo cha Shatta Wale kitakachotokana na kupigwa risasi Oktoba 18 (Jana) 2021.
Mtumishi huyo wa Mungu alipoulizwa namna tukio litakavyokuwa, alieleza kwa ufupi ya kuwa; kundi la watu wenye silaha watamvamia Shatta Wale na kumpiga risasi itakayomsababishia umauti huku akimsisitiza Shatta Wale kumtafuta ili amuombee na kumnusuru na kifo hicho.
Hii ina maana unabii wa Mtumishi wa Mungu umetimia au ni kiki kama za Meja Kunta?
Cc; @bakarimahundu