×

Maajabu! Kakakuona Aonekana Kibaha – Video

KIUMBE maarufu aina ya kakakuona ambae ni nadra sana kuonekana hadharani amekutwa katika eneo la Mpiji lililopo Maili Moja wilayani Kibaha mkoani Pwani nyumbani kwa mzee aliefahamika kwa jina la Mkwenya huku tukio hilo na kushudiwa na mamia ya watu waliofurika kujionea kiumbe huyo wa ajabu.

 

Ilikuwa jana Jumanne, Novemba 3, 2021 majira ya saa nne asubuhi ambapo idadi kubwa ya wananchi wanajitokeza nyumbani kwa mzee Makwenya lengo likiwa ni kujionea kiumbe wa ajabu ambae ni nadra sana kuoneakana machoni mwa watu.

 

Imezoeleka kuwa tangu enzi za mababu pindi anapoonekana mnyama huyu basi wakazi wa maeneo husika huweka vitu mbalimbali ikiwemo nafaka ikiwa ni ishara ya kupata ubashiri wa jambo litakalojitokeza kwa siku za mbeleni na hapa wakayafanya haya.

 

Wakati hili likichukuliwa kama jambo la kushangaza, lakini kwa wengine ni kawaida tu na hapa ni baada ya kufika kwa afisa wa wanyamapori ambaye alisema kuwa kila wanapopata taarifa za tukio la namna hiyo hufika na kisha kuwachukua viumbe hao ili kuwapatia hifadhi kama nyara ya serikali.

Leave a Comment