×

Mbunge Shabiby: “Waongezeni Mishahara Watumishi”-Video

Mbunge wa Gairo ,Ahmedy Shabiby ameitaka Serikali kuhakikisha kwamba ifikapo mwaka 2022 mishahara ya watumishi ambayo haijapandishwa kwa takriban miaka 6 mfululizo inaongezwa katika kiwango kinachostahili ili kuondoa hali mbaya ya uchumi.

Mbunge huyo amesema kwamba kwa mujibu wa utafiti wake binafsi watumishi ndiyo watumiaji wakubwa wa fedha na ambao husababisha fedha hiyo kuzunguka na kuwafikia watu wengine hivyo kuwaongezea fedha watumishi kutachochea kurejea kwa fedha mtaani.

 

“Mwalimu Nyerere alishawahi kusema maendeleo ya nchi yaendane na maendeleo ya watu, huwezi ukafanya maendeleo ya nchi bila Maendeleo ya watu ,leo tupo kwenye mpango wa bajeti Mheshimiwa Waziri wa Fedha, fanya maarifa yako ya aina yoyote 2022 ujue vyanzo utapata wapi sijui wapi.

Lakini hakikisha mishahara ya watumishi inapanda ,wala tusidanganyane nchi imekuwa na hali mbaya na watu wamezungumza maneno mengi sana ooh hela zimebanwa ,hela hazipo ,lakini mimi katika utafiti wangu nilichokuja kugundua ,bila watumishi kupandishiwa mishahara hali itazidi kuwa mbaya kwa watu wote “-Mbunge Shabiby.

Leave a Comment