×

Buchosa Wafurahishwa na Kauli ya Bashe

Buchosa. Wananchi wa Jimbo la Buchosa wilaya ya Sengerema mkoa wa Mwanza wamefurahishwa na kauli ya Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe aliyoitoa jana Ijumaa, Novemba 12, 2021 Bungeni Dodoma ya kutembelea Jimbo la Buchosa kwa lengo la kujionea skimu ya umwagiliaji ya Luchili iliyotelekezwa kwa muda mrefu sasa.

 

Hali hiyo imekuja baada ya Mbunge wa Jimbo la Buchosa, Mhe. Eric Shigongo kuzungumuzi Bungeni kuhusu kutelekezwa kwa skimu hiyo ambayo ilikuwa mkombozi kwa Wananchi wa Jimbo la Buchosa hasa katika kilimo cha zao ya mpunga na mahindi.

 

Mmoja wa wakazi wa Jimbo hilo Simoni Antony amesema ujio wa Naibu Waziri Bashe utafufua matumaini mapya ya wananchi wa Buchosa kuwa skimu hiyo itafufuliwa na kuwanufasha watanzania kwa ujumla.

 

Kwa sasa eneo ambalo ilikuwa skimu ya umwagiliaji mashamba hayo yanalimwa na baadhi ya wananchi hivyo wanaiomba Serikali kupitia Wizara ya Kilimo kuifufua skimu hiyo na kuweka mpangilio mzuri juu ya suala kilimo.

 

Mhe. Shigongo mara kwa mara amekuwa akipigania kufufuliwa skimu hiyo ambayo inauwezo mkubwa wa kuzalisha chakula kwa kupindi chote kutokana na kuwa kando kando mwa mwaziwa Victoria kutokana na upatikanaji wa maji ambap jana alihoji Bungeni.

 

“Skimu hiyo imetekelezwa kwa muda mrefu hivyo Serikali inatakiwa kuifufua kutokana na kilimo kuwa uti wa mgongo na asilimia kubwa wananchi wetu wanategemea kilimo, Mhe. Waziri yupo tayari kwenda jimboni Buchosa kujionea mradi huo ulivyotelekezwa?” amesema Shigongo.

 

Akijibu swali la Mhe Shigongo, Mhe. Bashe liwahakikishia wabunge wa majimbo ya Sengerema na Buchosa kuwa yuko tayari kutembelea majimbo hayo kujione mabwawa yalichimbwa Serikali jimbo la Sengerema na hayafanyi kazi kisha kutembelea skimu ya umwagiliaji ya Luchili iliyoko Buchosa ambayo imetekelezwa kwa muda mrefu.

 
 
 
 
 
View this post on Instagram
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 

A post shared by Global Publishers (@globalpublishers)

Leave a Comment