×

Wazee wa ‘Tuma kwa Namba Hii’, Wamtapeli Kikongwe Bilioni 1

WAKATI wale jamaa wa ‘tuma kwa namba hii’ wakiwa wamepungua Bongo, nakuletea hii kali kutoka Florida, nchini Marekani ambapo kikongwe mmoja wa miaka 82 ametapeliwa dola 700,000 ambazo ni zaidi ya shilingi bilioni moja!

 

Kwa mujibu wa maelezo ya kikongwe huyo, matapeli hao walimtafuta kwa njia ya simu na kumpatia taarifa ya kuugua kwa mjukuu wake ambaye walisema kuwa yupo kwenye hali mbaya na kumtaka kikongwe huyo atoe pesa bank na kumpatia dereva wa Uber  kwa ajili ya matibabu ya mjukuu wake.

 

Mamlaka ya upelelezi nchini humo imeiomba kampuni ya Uber itoe taarifa ya usafiri uliofika nyumbani kwa kikongwe huyo uliotumika kusafirisha fedha hizo, ili iwe rahisi kuwakamata matapeli waliohusika kumtapeli kikongwe huyo.

Cc; @bakarimahundu

Leave a Comment