
Mtu mmoja amekwama ardhini kwa zaidi ya siku tano baada ya kifusi cha mabaki ya machimbo ya dhahabu kushuka na kuziba upenyo wa shimo walilokuwa wakitumia kuingia ndani ya mgodi wa Mhalu, kitongoji cha Nyamatongo wilayani Kwimba mkoani Mwanza.
Emmanuel Issack, Mchimbaji Mdogo alikumbana na kadhia hiyo Novemba 7 huku wenzake wanane wakinusulika baada kukimbilia katika mashimo jirani ndani ya mgodi huo na kuokolewa baadaye na wachimbaji wengine waliokuwa nje.
Waziri wa madini Dotto Biteko amefika katika mgodi huo kuwafariji ndugu na wachimbaji huku akisisitiza juhudi zaidi kufanyika ili kumuokoa kijana huyo.