
IBRAAH au Chinga wa Konge Music anasema kuwa ana ndoto ya kutimiza kwa Tiwa Savage ambaye ni staa mkubwa wa muziki wa Nigeria.
Akizungumza na Gazeti la IJUMAA wiki kadhaa baada ya kusambaa kwa picha yake na Tiwa Savage wakiwa nchini Marekani, Ibraah anasema ndoto yake kubwa ya kutimiza iliyopo mbele yake ni kufanya kolabo na Tiwa Savage kutokana na ukubwa wake Afrika na duniani kwa jumla.
“Ni ndoto yangu ya kitambo sana, lakini sasa inakwenda kutimia,” anasema Ibraah anayekua kila kukicha kwenye gemu akiwa chini ya Harmonize.
Itakumbukwa kwamba mwaka 2017 Diamond alifanya kolabo na Tiwa Savage katika wimbo wake wa Fire ambao ulifanya vizuri Afrika na duniani.
STORI; KHADIJA BAKARI, DAR