×

Mke Amkata Korodani Mumewe

MWANAUME mmoja mwenye umri wa miaka 56 anauguza majeraha mabaya katika hospitali ya Nyambene kaunti ya Meru nchini kenya baada ya mkewe, mwenye umri wa kati ya miaka 40, kumkata korodani nyumbani kwao katika kijiji cha Akolone.

Mwanamke huyo, Karambu Meme inadaiwa alimshambulia mumewe Meme Kabati kwa madai kuwa hajawahi kumridhisha wanapokuwa katika tendo la ndoa.

 

Akithibitisha kisa hicho, Chifu Msaidizi wa eneo la Ntunene Edward Mutalii alisema kuwa baada ya kupokea habari hizo za kutatanisha, alienda kwa haraka eneo la tukio na kukuta sehemu ya korodani ya mwathiriwa ikiwa chini.

Polisi wamethibitisha kuwa Mwanamke huyo yuko rumande akisubiri kufikishwa mahakamani.

Leave a Comment