
SERIKALI ya Uholanzi imeanza kuwapeleka Wagonjwa wa Covid – 19 Nchini Ujerumani kutibiwa ili kupunguza msongamano kubwa unaozizonga Hospitali za Nchi hiyo zilizoko katika hali mbaya kutokana na ongezeko la Wagonjwa.
Leo Jumanne mgonjwa mmoja alisafirishwa kwa gari la wagonjwa kutoka mji wa Rotterdam na kupelekwa hospitali ya Bochum, Ujerumani, iliyoko kiasi kilomita 240 mashariki mwa nchi hiyo, na mgonjwa mwingine atasafirishwa baadaye leo.
Idadi ya wagonjwa wa Covid-19 katika hospitali za Uholanzi imeongezeka na kufikia kiwango kikubwa zaidi katika kipindi cha wiki za karibuni ambacho hakijawahi kuonekana tangu mwezi Mei.