×

Waziri Mkuu Afoka – “Hatutavumilia Vitendo Vyovyote Vya Ukatili”

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali itaendeleza mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsi na haitavumilia aina yoyote ya ukatili wa kijinsia utakaofanywa na mtu yeyote hapa nchini.

Waziri Mkuu Majaliwa amesema, Rais Samia Suluhu Hassan tayari amejipambanua na ameweka bayana msimamo wake dhidi ya ukatili wa kijinsia na kusisitiza umuhimu wa kubadili fikra na kufanya harakati zote kwa ushirika kati ya wanaume na wanawake ili kujenga jamii yenye amani upendo na usawa.

“Lazima jamii yetu ijenge msukumo wa kuhakikisha kuwa kila mtu katika nafasi yake anapaza sauti na kuchukua hatua ya kuzuia na kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia hususani ukatili wa kingono kama vile rushwa ya ngono, ukatili baina ya wenza, ubakaji, mimba na ndoa za utotoni”.

Leave a Comment