Mtoto Yunis ambaye anauwezo wa maajabu wa kutibu na kuponya watu kwa kutumia maji ya baraka amekutana na changamoto ya kuwekewa sumu kwenye chakula na kunusurika kifo na watu kutoka katika kijiji cha Bukama na wengine kutoka vijiji jirani.
Baba yake mzazi Fabian Ogot aeleza mambo mengi anayokutana nayo mtoto wao Yunis.