
WAREMBO wawili maarufu Bongo wanaozungumzwa zaidi juu ya ni nani anayejua kuvaa kuliko mwingine,
Fahyma na Paula Kajala; ubishi huo unakwenda kufikia mwisho ‘soon’.
Fahyma ambaye ni baby mama wa msanii Rayvanny aliyeporwa tonge kinywani na Paula; wawili hao wanawania
tuzo kwenye Kipengele cha Female Stylish Personaliy of the Year 2021 kupitia Tuzo za Swahili Fashion Week
zitakazofanyika Serena Hotel jijini Dar kati ya Desemba 3 hadi 5, 2021.

Pamoja na kwamba kuna wengine wakali kama Hamisa Mobeto na Jokate Mwegelo, lakini ushindani mkubwa unatajwa kuwa kwa Fahyma na Paula kutokana na kile kinachoendelea kati yao; kudaiwa ‘kushea’ mwanaume ambaye ni Rayvanny.
STORI; MWANDISHI WETU, DAR