×

Rais Museveni Kufanya Ziara Ya Kikazi Tanzania Leo

Rais wa Uganda, Yoweri Kaguta Museveni anatarajiwa kuwasili Tanzania kwa ziara ya Kitaifa kuanzia leo Novemba 27, 2021, na atapokelewa na Rais Samia Suluhu Hassan

Mbali na Marais hao kufanya mazungumzo, pia watashiriki ufunguzi wa kongamano la biashara kati ya Tanzania na Uganda

Rais Museveni atatembelea Bandari ya Dar na kukagua mradi unaoendelea wa SGR. Vilevile, ataenda Wilayani Chato, Mkoani Geita ambapo ataikabidhi rasmi Serikali ya Tanzania Shule ya Msingi iliyojengwa kwa ufadhili wake.

Leave a Comment