
MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Taifa na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni (KUB), Freeman Mbowe, ameshambuliwa na kujeruhiwa na watu wasiojulikana wakati akirejea nyumbani kwake Area D jijijini Dodoma.
Chadema imethibitisha na kusema amekimbizwa hospitali na anapatiwa matibabu.

“Ni kweli Mhe. Freeman Mbowe amevamiwa na watu watatu wakamkanyaga kanyaga na kumvunja mguu wa kulia kwa sasa yuko Ntyuka wodi no 4 na anaendelea vizuri, bado tunaendelea kuchunguza tutawajulisha baadaye,” – Gilles Muroto, RPC Dodoma.
