×

Tahadhari: Kirusi Kipya cha Corona

Shirika la Afya Duniani (WHO), Novemba 26, 2021 liliripoti uwepo wa aina mpya ya kirusi cha Uviko-19 kiitwacho “Omicron”, kinachosemekana kuwa na uwezo wa kusambaa haraka.

 

Kutokana na hali hiyo, Wizara ya Afya Tanzania imetoa tahadhari kwa Watanzania kuendelea kufuata ushauri wa wataalam wa afya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa huo.

 

Hatua hizo ni pamoja na kuchanja chanjo ya Uviko-19 ambazo zinatolewa bure kwenye vituo vya afya na kuepuka sehemu zenye mikusanyiko ya watu. Vile vile, uvaaji barakoa, kunawa mikono na sabuni kwa maji tiririka.

 

Leave a Comment