×

Rihanna Atangazwa Kuwa Shujaa wa Taifa

 

Mwimbaji Staa Rihanna ambae ni mzaliwa wa Barbados na Balozi wa kuitangaza Nchi hiyo ametangazwa rasmi kuwa Shujaa wa Nchi hiyo kutokana na kuitangaza Nchi yake na kujivunia wakati wote kuwa yeye ni mzaliwa wa visiwa hivyo vya Carribean.

Rihanna ametangazwa Shujaa kwenye sherehe Maalum za kusherehekea Barbados kuwa Jamhuri inayojitegemea tena yenye Rais wake baada ya miaka mingi ya kuongozwa na Ufalme wa Uingereza ambapo licha ya kuwa huru kwa miaka zaidi ya 50 Barbados iliendelea kuwa chini ya Malkia kama Mkuu wake wa Nchi hadi jana usiku.

Aliyekuwa Mwakilishi wa Malkia, Gavana-Jenerali Sandra Mason ambaye pia ni Mwanasheria wa zamani anayeheshimika Nchini humo ndiye ameapishwa kuwa Rais na Jaji Mkuu wa Barbados ikiwa ni miaka 55 kamili tangu Barbados ilipotangaza uhuru wake kutoka kwa Uingereza.

Leave a Comment