×

Kwa nini Mac Voice na Siyo Ibraah?

MAC Voice ni msanii mpya ambaye amedumu kwenye gemu ya Bongo Fleva yapata miezi mitatu tu chini ya Lebo ya Next Level ya msanii Rayvanny.

 

Katika kipindi hicho cha miezi mitatu, tayari Mac Voice ameanza kutajwa kuwania tuzo kubwakubwa duniani huku Ibraah kutoka Lebo ya Konde Gang ya Harmonize akiwa aonekani pamoja na kwamba amedumu kwenye gemu yapata mwaka mmoja na mizei kadhaa kuelekea miaka miwili sasa.

 

Mac Voice yumo kwente Tuzo za AEAUSA kwa kirefu African Entertainment Awards USA ambapo anawania tuzo hizo kwa mwaka 2021.

Mac Voice; katika tuzo hizo yumo kwenye Kipengele cha Msanii Bora Chipukizi mwaka 2021 ambapo atachuana na wasanii wengine kutoka nchi za Afrika wakiwemo Omah Lay, Liya Guchi, Oxlade, Jeeba, Ayra Starr na wengine wengi.

 

Wengi wanaamini kwamba, huwa msanii anapimwa kwa alichokifanya kwa mwaka mzima uliopita, lakini imekuwa tofauti kwa Mac Voice ndiyo maana watu wanajiuliza kwa nini Mac Voice na siyo Ibraah au Tommy Flavour ambao nao ni chipukizi waliofanya vizuri kwa mwaka mzima?

STORI; SIFAEL PAUL, DAR

Leave a Comment