
WANASAYANSI nchini Marekani kutoka Chuo cha Vermont, Chuo cha Tufts na Taasisi ya Baiolojia ya Wyss ya Chuo Kikuu cha Harvard wamegundua kuwa cell za xenobots zikikusanywa pamoja zinaweza kuzalisha roboti mwingine anayeishi kama kiumbe hai.
Ripoti kutoka CNN imesema kuwa Xenobots ni roboti iliyoundwa na mtaalam wa computer na maroboti Professor Josh Bongard kutoka chuo cha Vermont kwa kutumia chura kutoka Barani Afrika.
Roboti hii mpaka sasa bado ni cell inayoishi maabara na itakua tofauti na maroboti mengine yaliyoundwa kwa kutumia chuma na wana uwezo wa kuzaliana katika namna iliyo tofauti na mimea na wanyama
Mwaka jana baada ya kuzinduliwa, roboti hao walionesha uwezo wa kutembea, kufanya kazi, kujumuika na kujitibu pia. Lakini hamna mtu aliyetegemea kuwa wangeweza kuzaliana. Hata wanasayansi kutoka Tufts na Harvard ambao ndio walitengeneza roboti hizo wamepigwa na butwaa kuona roboti hizo zinaweza kuzaliana.

Michael Levin, Profesa wa Baiolojia na mkufunzi wa Kituo cha Utafiti cha Allen, aliongoza utafiti huo uliogundua kuwa roboti hizo zina uwezo wa kuzaliana lakini bado hata yeye mwenyewe mwanzoni hakuamini.
“Nilipigwa na butwaa anasema, chura wana jini ya kuzaliana wanayoitumia wenyewe lakini ukitoa seli zao kutoka kwenye kiini na kutoa nafasi kuziweka kwenye mazingira mapya, zinauwezo wa kutembea na kuzaliana…”
Ni wazi yakua roboti aliyeundwa kwa mateli amekuweko tangu zamani lakini kwa hili la aina hii ya roboti ni dhahili yakua teknolojia ya viumbe imekua.
SIFA ZA ROBOTI XENOBOTS
- Roboti xenobots huwa na ukubwa wa chini ya milimita moja
- Roboti xenobots ni wadogo sana kutosha kutembea kwenye mwili wa binadamu
- Wanafanya vitu vichache kama vile kutembea, kuogelea na kuweza kuishi bila kula kwa wiki
- Wanapenda kufanya kazi kwa makundi
Kwa kuhitimisha , hii inakua kama kitu nje ya muvi ya science fiction au hadithi. Akili ya bandia ni kitu chenye nguvu sana kinachotumika kwa huyu roboti. Ni maendeleo makubwa ambayo yatafungua milamgo kwa watafiti hapo baadae.