
KUELEKEA katika mchezo wa Derby ya Kariakoo, Mwenyekiti wa Simba, Murtaza Mangungu, amefunguka kuwa kwa namna alivyowatazama Yanga, anaamini Simba itaibuka na ushindi wa mapema Kesho Simba itakuwa
mwenyeji wa Yanga, kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara katika Uwanja wa Mkapa, Dar.
Akizungumza na Championi Ijumaa, Mangungu alisema kwenye mchezo wa kesho timu hiyo
inaingia uwanjani kucheza mchezo wa ligi bila hofu kwani hawaitambui Yanga tena kama wapinzani wao hivyo wanaenda kucheza na timu kama zile za daraja la kwanza au la pili tu.
“Tayari maandalizi ya timu yako vyema na kubwa tunashukuru mchezo huu hautakuwa na presha ya aina yoyote kwetu, kwani tayari Yanga ni timu ya kawaida tu kwetu kwa sasa maana tayari hatuwatambui kama wapinzani wetu kwa ninachojaribu kufanya ni kupunguza matatizo ambayo yapo kwenye kikosi changu ambayo yalikuwepo tangu kuanza kwa msimu huu, ikiwemo washambuliaji kushindwa kufunga mabao.”
Geita wapo nafasi ya 15, baada ya kucheza mechi 8 wakiwa na pointi 5 kwenye msimamo. sababu dabi yao sasa ni dhidi ya Azam FC.
“Wameona ukubwa wetu na ndiyo maana wamejitoa mapema kabisa, hivyo sisi tutaendelea kuwahesabu kama timu
nyingine za kawaida za daraja la kwanza au la pili na zaidi mchezo huu tunaenda kushinda mapema tu kwani timu yetu imekamilika kila idara,” alisema Mangungu
Stori: Musa Mateja, Dar es Salaam