×

Faru Rajabu Mtoto wa Faru John Kuoa Kenya – Video

MTOTO wa Faru John, maarufu kama Faru Rajabu huenda akapata ‘jiko’ jingine siku za hivi karibuni baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kufikia makubaliano na kiongozi mwenzake, Rais wa Kenya kupata Faru majike kwa ajili ya wanyama hao waliopo katika hifadhi ya taifa ya Serengeti.

 
Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari baada ya kikao cha ndani na Rais Kenyatta, Rais Samia amesema kuna Faru wawili katika mbuga za taifa na hawana wake.
 
“Nimemwambia Rais Kenyatta kwenye mbuga zangu kule Ngorongoro pengine na Serengeti nina madume wawili wa Faru hawana wake, hawana wenza sio vibaya hawa Mafaru wakaoa Kenya sisi tuko tayari kutoa mahari tupate mafaru jike wa Kenya waolewe Tanzania,” amesema Rais Samia na kuongeza, “Mdogo wangu amenikubalia na siku ya kuwapokea lazima tukate keki.”

Hayo yamesemwa leo Ijumaa Desemba 10, 2021 na Rais Samia Suluhu Hassan wakati akifafanua baadhi ya maeneo ambayo yamewekewa makubaliano kati ya nchi hizo mbili ikiwemo utalii, nishati, ulinzi wa mipaka na sekta ya afya

 

Katika sekta ya utalii, Samia amesema ikolojia ya Tanzania na Kenya ni moja ila imegawanywa na mipaka huku akibainisha kuwa wamewataka mawaziri wa eneo hilo kukaa, kuzungumza na kuondosha changamoto ili nchi zifaidike kuleta watalii wengi na kupata mapato.

 

Aidha, Samia amempatia Kenyattandege aina ya Korongo 20 kama zawadi ya Kristimas. Ndege 20 waliotolewa kwa Kenya kutaifanya nchi hiyo kuwa na ndege hao 32 kutoka 12 waliopo sasa kwani Tanzania ilikuwa nao 4000.

 

Amesema sekta hiyo kwa upande wa Kenya walikuwa wakiona ndege korongo wakiwa Tanzania na wakati mwingine katika kutembeza watalii walikuwa wakiwaulizia lakini hawapo nchini kwao hivyo ilibidi watalii watembee kuja Tanzania.

 

Leave a Comment